RAY THE GREATEST

TANGAZO LA KUBADILISHA JINA LA BLOGU

TANGAZO LA KUBADILISHA JINA LA  BLOGU
Tunawaomba radhi wadau wote wa blogu ya RAY THE GRETEST kuwa tumebadilisga jina la Blogu na sasa inaitwa:-www.raythegreatest.blogspot.com

Thursday, September 10, 2009

KAZI IMEPAMBA MOTO NDUGU WADAU


Hapo ndio mnapofurah ndugu wadau katika kupata mashoot ya kumwaga katika filam,Akionekana camera men Farid Wezi katika kutayarisha mzigo mpya

WADAU MZIGO MPYA UKIWA JIKONI UNATAYARISHWA


Mzigo mpya ukitayarishwa ukiwa na yule actress nileyewatambulisha pale mwanzoni,Hapa akionekana akielekezwa kitu

WASANII TULITOA SAPOTI YA KUTOSHA KWA MSANII MWENZETU


Wadau na mimi ndugu yenu sikuwa mbali na mshikaji wangu Kanumba katika kumpa sapoti kwa kutuwakilisha vyema ndani ya nyumba ya BBA4 Revolution,Kushoto kwangu ni Joyce Kiria na Mahsein Awadh


JB naye alikuwepo ndani ya Tamal Hotel kumpa sapoti  mshkaji,Hapa akitoa nasaha kidogo



KANUMBA AKIWA NA MTAYARISHAJI WA BONGO MOVIE


Mtayarishaji wa Bongo movie akuwa mbali katika kutoa sapoti kwa Kanunba ndani ya Hotel ya Tamal Mwenge

MUDA MFUPI BAADA KANUMBA YA KUWASILI KUTOKA SOUTH AFRIKA BBA 4




Ilikuwa ni muda mfupi baada ya kutua ndani ya bongo kutoka south  afrika,Kanumba akiwa na baadhi ya maactress ndani ya Hotel ya Tamal alikofanyiwa pati na wasanii wenzake,mwana alitoka bomba sana

Monday, September 7, 2009

UPANDE WA PILI MJENGONI RJ COMPANY TZ LTD


Nje ya mjengo

Ndani ya Mjengo

Ofisini kwa Mkurugenzi.

ASUBUHI YA LEO TUMESHINDWA KUFANYA SHOOTING KWA AJILI YA UMEME ULIOKATIKA KUANZIA ASUBUHI MPAKA JIONI


Wahusika wakuu wa Movie mpya iliyotaka kuanza kushutiwa leo Hemed na monica

Wasanii bado wakiwa wanasubiri kurudi kwa umeme,huwezi amini hakukufanyika kitu leo tukisubiri umeme siku nzima

Mawazo ya kuondoka yalinijia,nikishauriana na wenzangu tuondoke.

Sunday, September 6, 2009

MIMI PIA NILIKUWAMO JAMANI KUWAKILISHA !!!!!!!!!!


Ndani ya Paradise City Hotel (Mafuta House) usiku wa kuamkia leo katika uzinduzi wa BBA 4 Revolution ulioandaliwa na Multchoice Tanzania.Mpaka tunaondoaka hatujui muwakilishi wetu ni  nani katika shindano hili!!!!

KANUMBA AKIWA NA WAKILISHI WA BBA4 WALIOINGIA USIKU WA LEO


Washiriki wa BBA 4 wakipata chakula,Mwenye shati la pink ni KANUMBA

KANUMBA NDANI YA BBA 4 REVOLUTION


Kanumba akiwa ndani ya BBA 4 Revolution akiwa kama mwakilishi wa watu maarufu kutoka Tanzania,Tunashukuru mungu kwa nafasi hii aliyoipata ndugu yetu Kanumba,Akhsante sana Movie Magic kwa kufanya mpaka ndugu yetu kupata nafasi hii,Watanzania watambue kwamba Kanumba siyo mwakilishi katika shindano hilo,Mwakilishi wa Tanzania atajulikana hivi karibuni

HAPA KIKAO KINAENDELEA


Kikao kilikuwa kikali sana kama mnavyoona ndugu wadau, JB nae hakubaki nyuma wasanii tunasema mbele daima nyuma mwiko

BAADHI YA WASANII WAKIJADILI MAMBO FULANI KABLA YA KUINGIA KWENYE KIKAO


Kama mnavyoona wasanii wa kiwanda cha movie Tanzania wakiwa na hasira za kuibiwa kazi zao,Single mtambalike(Richie)mwenye tisheti nyekundu,Mahsen awadh(Dr cheni) mwenye shati la blue lenye mistari na bishop mwenye shati la blue jamani imetosha sasa kuibiwa kazi zetu na sisi tunataka kuwa kama mastaa wa Hollywood...

JAMANI HAWA NDIO WASANII WA BONGO KATIKA KIKAO LAMADA


Wadau na wasanii na maproducer wakiwa katika kikao cha kutokomeza uharamia wa kazi zao,jamani tumechoka kuibiwa kazi zetu

Saturday, September 5, 2009

NAWASHUKURU WADAU AMBAO WANANITEMBELEAGA NIKIWA KAZINI


Hawa ni baadhi ya Wadau wanaonitembeleaga nikiwa kazini kama unavyoona wakiwa nyuma ya kamera wakicheki maswala yote ya uendeshaji,nawashkuru sana.

KWA WANAOMKUMBUKA HUYU DADA ENZI ZIIIIIILE "RAYUU"


Wadau huyu dada alipotea sana kwa wanaokumkumbuka enzi za Kaole alikuwa anatisha,RJ Company Inamrudisha tena ndani ya kiwanda hiki cha Movies anakuja na Movie kali sana......!!!!

KAKA CHIKOKA A.K.A CHOPA MCHOPANGA


Dr. Chopa akiwa kazini ndani ya Movie Jina..........Msubirini kijana anakuja na mambo matam mengi tu!!!!!!!!

JAMANI SANAA YETU HII SI HABA INATULIPA KIDOGO


Jamani movie za bongo zinalipa kidogo wadau hapa  kama mnavyomuona Johari si haba nae anajimuvuzisha taraaatiiibu.

SHE'S ONE OF THE TALENTED MOVIE STAR IN BONGO


Muite Blandina Chagula,Kalunde,Namande alimaarufu JOHARI nani asiyemjua huyu dada kwa hisia za kulia unapomkuta akiwa kazini .

MAMAA SANDRA NA YUSUPH MLELA ON SET



Wasanii Yusuph Mlela na Mamaa Sandra on set ndani ya Divorce, nashkuru sana kwa kazi nzuri milioinyesha ndugu zangu.nawakubali sana

BAADHI YA WAREMBO WANAOPATIKANA NDANI YA MOVIE YA "DIVORCE"


Hawa ni baadhi ya casting wanaopatikana ndani ya movie ya Divorce.

BAADA YA "DIVORCE" INAYOTOKA 29/9/2009,KAA TAYARI KWA "FAIR DECISION"


Wandugu nawatangulizia movie nyingine hiyo ambayo iko jikoni inapikwa "Fair Decion" itatoka soon baada ya "Dirvoce" ambayo itakuwa madukani kuanzia tarehe 29/9/2009. sina mengi saana itakapotoka pata nakala yako.

RJ Company Tanzania Ltd,Karibuni Wadau


Mjengo huo unaouona hapo ni RJ Company Tanzania Ltd,Wadau hapa ndipo kazi zote za utengenezaji wa filim za kibongo nyingi ambazo nimecheza mimi na wasanii ambao nimeshirikiana nao,hivyo wadau kama kuna yoyote anayetaka kufanya kazi na RJ  mnakaribishwa.Kaa tayari mdau kwa uzinduzi rasmi tarehe na lini nitawajia rasmi.

NAWASHKURU WADAU WOTE KWA MAONI


Nashkuru sana kwa maoni yenu wadau mmeonyesha uzalendo kwangu,nachopenda kuwaahidi ni kujitahidi kuiboresha blog hii kama mnavyojua mwanzo ni mgumu ndugu zangu ila mtapata update za kutosha wote mlionitumia maoni nashkuru sana.

Wednesday, September 2, 2009

MAINDA ONE OF THE BEST ACTRESS




Wadau wengi nadhani mtakuwa mnnakubali ukali wa huuyu mwanadada katika gemu zima la movie za bongo anakipaji kwakweli

THE NEW ACTRESS IN TOWN!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


Wadau kaeni mkao wa kula RJ Company Tanzania Ltd inashuka na actress wa ukweli
Jina:...... Movie:......
Hivyo basi kaeni mkitulia na kusubiri mambo mazuri kutoka kwa huyu dada.

ON SCENE WITH MY BROTHER "MAGARI" KATIKA DIVORCE COMMING SOON!!!!!


Mzee wa kisauti Mr Magari with me the most great (Ray) on location
Wadau kaeni mkao wa kula "Divorce"

KANUMBA "THE GREAT" AND RAY "THE GREATEST"


Nipo na Swahiba wangu mkubwa Kanumba "The Great" lakini mimi ndio "The greatest wake
na analitambua hilo much love brother!!!!!!!!!!!!!!!! hapa kwenye kushoot movie ya Oprah one of the best movie in Bongo.

"DIVORCE" COMING SOON!!!!!!


Divorce one of the great movie comming soon, produced by RJ Company
Dont miss it go and get your copy,staring Me,Sandra,Johari and Mlela 



WELLCOME TO MY WORLD "RAY THE MOST GREAT"


Karibuni wadau katika blogu yangu hii, humu utapata kujua mambo mbalimbali yahusuyo mimi Ray "the most great" katika swala zima la Enterntiment expecial Movies na maisha kwa ujumla.