RAY THE GREATEST

TANGAZO LA KUBADILISHA JINA LA BLOGU

TANGAZO LA KUBADILISHA JINA LA  BLOGU
Tunawaomba radhi wadau wote wa blogu ya RAY THE GRETEST kuwa tumebadilisga jina la Blogu na sasa inaitwa:-www.raythegreatest.blogspot.com

Thursday, September 10, 2009

WASANII TULITOA SAPOTI YA KUTOSHA KWA MSANII MWENZETU


Wadau na mimi ndugu yenu sikuwa mbali na mshikaji wangu Kanumba katika kumpa sapoti kwa kutuwakilisha vyema ndani ya nyumba ya BBA4 Revolution,Kushoto kwangu ni Joyce Kiria na Mahsein Awadh


JB naye alikuwepo ndani ya Tamal Hotel kumpa sapoti  mshkaji,Hapa akitoa nasaha kidogo



2 comments:

Anonymous said...

Ray jana nilikiuwa naangalia kipindi cha Bongo Movie lakini kwa bahati mbaya nilichoshwa na kukerwa na majigambo mliyokuwa mkiyatoa pamoja na hali ya kiubaguzi ambayo mliidhihirisha.(kwa walioangalia kipindi wataelewa ninachokimaanisha. Napenda uelewe wewe na wasanii wenzako ni wafanyabiashara hivyo ili kufanikiwa mnatakiwa mzikubali changa moto mbalimbali zinazokuja kwenu ikiwemo ya kukosolewa kuhusu kugha ya kiingereza na na nyinginezo.
Mmmeanza kujitenga na watangazaji wa redio na wasanii wenzenu wa komedi kesho itakuja kujitenga kati ya Ray na JB mpaka mwisho huo mnaouita umoja utaweza sambaratika, rejea hotuba ya baba wa taifa inayozungumzia dhambi ya ubaguzi na utaelewa ninachosema.
Ze comedy kutumia mjadala uliopo hivi sasa juu ya ushiriki wa Kanumba BBA ni sehemu ya kazi yao maana ndio issue inayo "hit"kwasasa na wao ili wachekeshe ni lazima wapate mtu mmoja kwenye jamii ambaye amefanya jambo eidha la kuchekesha au lisiloendana na hadhi yake ndio wapate stori ya kufanyia shooting, kwahiyo si vizuri kuwachukulia kama ni watu waliomkebehi Kanumba. Mbona mara kadhaa wamewaigiza viongozi wakuu wa nchi akiwemo Rais na hamkusema lolote? Elewa mnapigania kuwa wasanii wa kimataifa na duniani kote inaeleweka kuwa kiingereza ndio lugha ya kibiashara kwahiyo si vizuri kurumbana na wanaowakosoa, jambo la busara ni kukaa chini na kutathmini je ni kweli mwenzenu alikosea? na kama ndio nini kifanyike ili hali hiyo isijirudie siku za usoni lakini si malumbano ambayo naamini hayatowasaidia na badala yake mtaishia hapahapa nyumbani tu. Kutokubali changamoto kutawafanya muwe watu wakuchemsha kila siku kama inavyodhihirika kwenye baadhi ya filamu zenu ambamo utakuta muigizaji maarufu anakunywa juisi kwa glasi ya wine, au ana kula wali kwa kijiko badala ya uma na filamu hiyo inaonekana dunia nzima kupitia AFRIKA MAGIC +, ni vitu vidogo lakini kwa wasanii mnaotaka mfike mbali vinaathari kubwa kibiashara.
SAMAHANI KAMA KWA MAONI HAYA NITA MKWAZA MTU YEYOTE. Ahsante.

Anonymous said...

wee cheni waongea na nani tena unatuumiza wenzio uku.